The House of Favourite Newspapers

Sekretarieti ya ajira yaelezea mafanikio ya Tehama

0

  1.Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma,Riziki Abraham (kushoto) akiwa na Kaimu Katibu wa TEHAMA, Mtage Ugullum wakati akitoa taarifa yake.Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, Riziki Abraham (kushoto) akiwa na Kaimu Katibu wa TEHAMA, Mtage Ugullum, wakati akitoa taarifa yake.

2.Viongozi hao wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).Viongozi hao wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).

3.Wanahabari wakichukua tukio hilo.Wanahabari wakichukua matukio jatuja hafla hiyo.

OFISI ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma leo imeeleza mafanikio na namna inavyotumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kuboresha na kurahisisha  mchakato wa ajira kwa kutangaza nafasi za kazi, kupokea maombi, hata kuwaita kwenye wahusika kwenye usaili,  kuwapa taarifa mbalimbali za kazi na kuwawezesha waombaji kazi kutumia teknolojioa ya mfumo huo.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Habari Serikalini, katika sekretarieti hiyo,  Riziki Abraham, alisema kuwa kitengo hicho kimepewa dhamana ya kuendesha mchakato wa ajira kwa niaba ya waajiri mbalimbali serikalini.

Ameeleza katika kuwawezesha wananchi hususani waombaji fursa za ajira pamoja na kutumia tovuti yao ya www.go.tz kupata taarifa kwa wakati na uhakika,  sasa ofisi yao imekuja na mifumo mingine miwili ya kielektroniki ili kuhakikisha maombi yote na taarifa mbalimbali za waombaji wa fursa za ajira yanapokelewa haraka  miongoni mwa wananchi hususani waishio pembezoni mwa jiji na waishio nje ya mipaka ya Tanzania.

Ameitaja mifumo hiyo kuwa ni mfumo wa kuomba fursa za ajira unaojulikana kama ’’recruitment portal’’ na unaopatikana kwa anuani ya “portal.ajira.go.tz” na mfumo wa pili ni kwa ajili ya kupata ujumbe wa papo kwa papo kupitia simu za kiganjani ujulikanao kama “Job alert system” kwa kubofya *152*00# kisha kufuata maelekezo.

Aidha  alielezea sababu za kuanza kutumia mifumo hiyo miwili kwamba ni  kulenga kupunguza changamoto zilizokuwepo yakiwemo malalamiko ya waombaji fursa za ajira kuhusu upotevu wa maombi yao ya kazi, yaani mchakato wa ajira na taarifa zao uliokuwa ukichukua muda mrefu zaidi ya siku tisini.

Vilevile alisema kuwa hadi kufikia Mei 29 mwaka huu jumla ya waombaji waliojiandikisha kwenye mfumo mpya wa utumiaji maombi ya kazi walikuwa 97,765 huku 89,484 wamejiunga kwenye mfumo wa kupata taarifa za uwepo wa fursa za ajira kupitia simu zao za kiganjani na baruapepe.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply