The House of Favourite Newspapers

Semina Kubwa ya Ujasiriamali Kufanyika Keshokutwa Dar Live

wezesha5

Meneja Mkuu wa Wezesha Mzawa, taasisi ya kifedha inayojihusisha na mikopo kwa wajasiriamali, Samson Lwiza (kushoto) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) leo katika ofisi za Global Publishers Ltd, Bamaga – Mwenge jijini Dar. Katikati ni Mweka Hazina wa Wezesha, Shamimu Mshana akiwa na Ofisa Mikopo wa taasisi hiyo, Glory Minja (kulia).

wezesha-1

Samson Lwiza (kushoto) akiendelea kueleza juu ya semina hiyo kubwa ya ujasiriamali inayotarajiwa kufanyika keshokutwa katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem.

wezesha-3

Samson Lwiza (kushoto) akisikiliza maswaki kutoka kwa wanahabari (hawapo pichani).

wezesha1

Mkutano wa Wezesha na wanahabari ukiendelea.

wezesha-mzawa

Timu ya Wezesha Mzawa ikiwa katika pozi baada ya mkutano huo.

DAR ES SALAAM: Semina kubwa ya ujasiriamali inatarajiwa kufanyika keshokutwa (Jumamosi) Desemba 17, 2016 katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem jijini Dar ambayo itawakutanisha pamoja mabingwa wa kuhamasisha watu kujikomboa kiuchumi.

Miongoni mwa watakaotoa mada kwenye semina hiyo ambayo haina kiingilio, ni Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo ambaye anafahamika kwa uwezo wake wa kutoa mafunzo yenye mifano, iliyowafaidisha wengi kote Tanzania.

Meneja Mkuu wa Wezesha Mzawa, taasisi ya kifedha inayojihusisha na mikopo kwa wajasiriamali, Samson Lwiza, ambao ndiyo wadhamini wa semina hiyo, alisema watu wengine watakaotoa mada siku hiyo ni Hassan Ngoma, Mushi Macmilan na Dk. Didas Lunyungu.

“Sisi licha ya kufadhili semina hiyo, lakini pia siku hiyo tutatoa mada kwa washiriki jinsi gani wanaweza kujipatia mikopo yenye riba nafuu kutoka kwetu. Tutawaeleza pia namna mtu unavyoweza kujikomboa kiuchumi kutoka kwenye mtaji mdogo,” alisema Lwiza.

Semina hiyo itaanza saa 2.30 asubuhi ya Jumamosi hadi saa kumi na moja jioni na inatarajiwa kuhudhuriwa na wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

Comments are closed.