The House of Favourite Newspapers

Serena: Sina mimba ya Drake

serena-williams1-(1)Mcheza tenisi namba moja duniani, Serena Williams.

New York, Marekani
TAARIFA zilizoenea kwa kasi kuwa mcheza tenisi namba moja duniani, Serena Williams ana ujauzito wa rapa Drake Graham, zimekanushwa vikali.

MAIN-A-history-of-serena-and-drakes-romance-over-the-yearsHivi karibuni, iliripotiwa kuwa Serena tayari ameshanasa ujauzito wa Drake na kwamba dalili zote za mimba kwa mlimbwende huyo zimeanza kubainika kabla ya hivi karibuni watu wa karibu na staa huyo kueleza ukweli juu ya suala hilo.

“Serena hajafurahishwa na taarifa hizi zinazopotosha, huwa anatuambia jinsi gani anajisikia. Ukweli ni kwamba hana ujauzito na ni muda mfupi tangu akutane na Drake kwenye ‘event’ moja kubwa New York, kwa kifupi hakuna ukweli wowote,” alisema mmoja wa marafiki wa karibu na Serena.

Comments are closed.