The House of Favourite Newspapers

SERENGETI ILIVYOJITOA KATIKA JAMII

Meneja Mawasiliano Imani Lwinga akitoa somo.

Kampuni ya Serengeti Breweries leo imefanya mkutano na wanahabari na kujadiliana mambo kadhaa. Akizungumza kwenye mkutano huo, Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Imani Lwinga amesema kupitia mpango wao wa IQ wamewataka wateja wao kunywa kistaarabu ili kuweza kuyamudu vyema majukumu mengine ya kujenga taifa. Lwinga amesema unywaji wa pombe una faida nyingi ukizingatia masharti lakini pia una madhara kama hautakunywa kwa kuzingatia unywaji wa kistaarabu.

Wanahabari wakifuatilia kwa umakini mkutano huo.

Naye Meneja ushirika wa kampuni hiyo, John Wanyancha amesema kampuni hiyo imeanza kufanyakazi na wakulima wa hapa nchini. Amesema wamekuwa wakiwaelemisha kilimo bora cha malighafi wanazotengenezea bia za serengeti nao wamekuwa wakizinunua na kuepuka kuagiza malighafi nje ya nchi kama ilivyokuwa awali.

Baadhi ya bia zinazotengenezwa na kiwanda hicho.

Wanyancha amesema sambamba na hilo wamekuwa wakitoa misaada ya kijamii kama vile kuchimba visima virefu na kutatua matatizo ya maji katika jamii ambapo mpaka sasa wameshawakomboa wananchi zaidi ya mbili kwa kuwapa maji bure.

 

Sambamba na hilo Wanyancha amesema wamekuwa wakitoa skolaship kwa watoto wa wakulima wanaofanya nao kazi kwa kuwasomesha vyuo vikuu mbalimbali ikiwemo vya nje.

Meneja Ushirika wa kampuni hiyo, John Wanyancha akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Usikivu ukiendelea.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL

Comments are closed.