The House of Favourite Newspapers

SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA VIWANDA VYA NGUO ILI KUKIDHI SOKO LA NDANI

Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage,(kulia) akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo baada ya hafla hiyo kuisha.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Growth Trust, Oliver akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.
Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.

SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuthamini wajasiriamali wa viwanda vya kutengeneza nguo hapa nchini vinavyoendelea kukua na kukidhi mahitaji ya wanachi.

 

Hayo yameelezwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, wakati wa sherehe ya kutimiza miaka 25 ya taasisi ya TGT iliyofanyika katika Viwanja vya Makumbusho ya  Taifa  Posta jijini Dar es Salaam.

 

Taasisi hiyo inayojishughulisha na masuala ya wajasiriamali, pi imebadilisha jina la mwanzo kutoka Tanzania Gatsbay Trust na kuwa Tanzania Growth Trust.

 

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Growth Trust, Oliver Lwena amesema kuwa lengo la taasisi yake ni kuendelea kufundisha wajasiriamali wadogo kwa wakubwa ili kutengeneza ufanisi wa kujikwamua kiuchumi na maemdeleo na hasa elimu ya juu ya masuala ya kibiashara.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.