The House of Favourite Newspapers

Serikali Kuja Wiki ya Uchanjaji wa Corona

0

MSEMAJI Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Serikali ipo mbioni kuaandaa utaratibu wa wiki ya uchanjaji ambayo inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Septemba au mwanzoni mwa mwezi Oktoba, Msigwa ameyasema hayo leo Jumapili Septemba 12, 2021 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya wiki.

 

”Serikali moja ya vitu ambayo inaviangalia kwasasa ni kuhakikisha tunakuwa na wiki ya uchanjaji, utaratibu huu sasa unaandaliwa bila shaka mwishoni mwa mwezi wa 9 au mwanzoni mwa mwezi wa 10, tutakuwa na wiki ya uchanjaji, ambapo viongozi wa nchi nzima watashiriki kwenye wiki hivyo kuhakikisha watanzania wengi wanapata chanjo,” amesema Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali.

 

Aidha ameeleza kuwa ”Wataalam wetu wanatuambia watu ambao hawajachanjwa wakiugua Uviko-19 wanapata madhara makubwa na wengine wanapoteza maisha lakini waliochanjwa wanatibiwa na wanarudi nyumbani”.

Leave A Reply