The House of Favourite Newspapers

Serikali Yaagiza Televisheni Kufungwa Mahospitalini

0

Serikali imewaagiza Waganga Wakuu wote nchini kuweka Televisheni na vipeperushi katika vituo vya kutolea huduma za afya hususani majengo yanayowahuduma akina Mama Wajawazito na kuweka vipindi vinavyoelimisha akina Mama juu ya afya za uzazi na jinsi ya kujikinga na magonjwa.

 

Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Leonard Subi wakati akizungumza na Wataalamu wa Afya katika Kituo cha Afya Kaloleni, Arusha.

 

“Naagiza Waganga Wakuu wote nchini kununua na kuweka Televisheni katika vituo vya kutolea huduma za afya na Hospitali ili kuwapatia fursa akina Mama kujifunza afya ya uzazi ikiwa ni njia ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito,” Dk Subi.

Leave A Reply