The House of Favourite Newspapers

SERIKALI YAKANUSHA KUIUZA NDEGE YAKE YA AIRBUS NCHINI KENYA

SERIKALI imekanusha taarifa za uvumi zinazosambaa mitandaoni zikidai ndege mpya aina Airbus 220-300 iliyowasili nchini mwishoni mwa mwaka jana kuwa imepelekwa nchini Kenya kwa ajili ya kuuzwa.

Serikali imesema habari hiyo ni ya uongo na uzishi, hivyo wananchi waipuuze na kwamba ndege hiyo ilikodiwa na Kampuni ya AIRBUS kutoka kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa ajili ya maonyesho (Airshow) jijini Nairobi kwa sababu, hakuna ndege kama hiyo Barani Afrika isipokuwa Tanzania pekee, hivyo mashirika mengi ya ndege kutoka nchi mbalimbali yanakuja kuiona Airbus ya Tanzania ili na wao waweze kuagiza. 

Kwa hiyo kilichofanyika ni suala la masoko na kuinadi zaidi yetu na kwamba tayari imerejea nchini jana, Alhamisi, Machi 28, 2019, usiku kuendelea na safari zake.

Comments are closed.