The House of Favourite Newspapers

Serikali Yasaini Mikataba Saba ya ujenzi wa Barabara ya Sh. 3.7 trilioni

0

SERIKALI ya Tanzania chini ya usimamizi wa Wakala wa barabara nchini (TANROAD) imsaini mitakaba 7 ya ujenzi wa barabara 7 kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 2035 ya thamani ya shilingi tirioni 3.775 na kukamilika kwa muda wa miaka 4 tangu sasa.

Hayo yameeleza Juni 16, 2023 na Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Mhandisi Makame Mbarawa wakati wa uwekaji wa sahihi katika mikataba hiyo iliyofanyika ukumbi wa jakaya Kikwetwe jijini Dodoma.

Mhandisi Mbarawa amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2022/23 Wizara ilianza taratibu za manunuzi kwa ajili ya kuwapata Makandarasi wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara saba (7) zenye jumla ya kilometa 2,035 kwa kutumia utaratibu wa Engineering, Procurement, Construction and Financing (EPC + F).

Amsema kuwa Barabara hizo zitafungua fursa za kiuchumi katika maeneo zinapopita na kwa Taifa kwa ujumla.

“Hatua iliyofikiwa hadi sasa ni kuwa Makandarasi wa miradi yote saba (7) wamepatikana ambapo leo hii tumeshuhudia Utiaji Saini wa mikataba ya kazi za ujenzi wa miradi hiyo.”

Amezitaja barabara hizo kuwa zitajengwa kwa utaratibu huu wa EPC + F ni barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435.8), Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa (km 453.42), Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 384.33).

Amezitaja barabara nyingine kuwa ni barabara ya ya Igawa – Songwe – Tunduma (njia nne) (km 237.9), Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175), Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 339) na Barabara ya Mafinga – Mtwango – Mgololo (km 81).

Mhandisi Mbarawa amesema kuwa maeneo mengi ambayo barabara hizi zitapita yana rasilimali nyingi ambazo hazichangii ipasavyo katika uchumi wa nchi kama inavyopaswa kuwa kwa kutofikika kirahisi kutokana na ukosefu wa barabara zinazopitika wakati wote wa mwaka.

“Hivyo, Serikali inafanya jitihada za makusudi kuhakikisha kuwa maeneo yote ya kimkakati kiuchumi yanafikika kwa urahisi ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.

“Aidha, barabara hizi zitachochea kiu ya matumizi ya bandari zetu kwa nchi jirani za Zambia, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zimbabwe, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini hivyo kuinua ukuaji wa makusanyo ya fedha kupitia Bandari zetu” ameeleza Mhandisi Mbrawa.

Aidha Mhandisi Mbarawa ameeleza kuwa barabara hizo zitarahisisha usafiri wa wananchi na usafirishaji wa mazao ya misitu, mazao ya biashara, mazao ya chakula, mazao ya uvuvi na ufugaji, malighafi za madini kama vile makaa ya mawe, grafaiti na chuma kutoka mikoa ya Kusini kwenda katika masoko ya ndani na nje ya nchi na kuchochea kasi ya uzalishaji wa mazao hayo na ongezeko la mapato ya Serikali.

Akizungumzia faida za barabara hizo amesema kuwa barabara hizo zitachochea kiu ya matumizi ya bandari za Tanzania kwa nchi jirani za Zambia, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zimbabwe, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini hivyo kuinua ukuaji wa makusanyo ya fedha kupitia Bandari zetu.

Ameeleza kuwa Serikli inatarajia ujenzi wa barabara hizo utakapokamilika, maeneo yote yenye mikakati mizuri ya kiuchumi yatavutia kwa kiwango kikubwa uwekezaji wa ndani na kimataifa na kuzalisha ajira kwa Watanzania.

SANDALAND – “JEZI MPYA ya SIMBA HAIJAWAHI KUTOKEA, HAWATAGOMBANIA WALA KUPIGANIA JEZI”…

Leave A Reply