The House of Favourite Newspapers

Serikali Yatangaza Tenda Ujenzi wa Barabara za Jiji la Arusha, Stendi na Masoko Vinakuja – Video

0

Serikali kupitia Wizara ya Rais TAMISEMI imetangaza rasmi tenda ya ujenzi wa barabara tatu za Jiji la Arusha kwa kiwango cha lami.

Tenda hiyo imetangazwa leo Jumanne, Februari 28, 2023 kupitia gazeti la Serikali la Daily News ambapo mradi huo unajengwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia. Barabara zitakazojengwa ni Engosheraton, Olasiti na Oljoro mpaka eneo panapotarajiwa kujengwa stendi mpya ya jiji la Arusha.

Akizungumzia hilo, Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo amesema barabara hizo ni mhimu kwa uchumi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kwani zimekuwa kichocheo kikubwa cha kibiashara na utalii kwa jiji hilo la utalii barani Afrika.

Gambo amesema pia kuwa, baada ya barabara hizo, kinachofuata sasa ni stendi kuu mpya na ya kisasa ya Jiji la Arusha, kisha soko la kisasa la Kwamrombo na Soko la Kilombero.

“Kilio kikubwa cha wananchi ni stendi ya kisasa, michakato yote iko vizuri na hatua inayofuata wizi mbili zijazo kuanzia leo itatangazwa tenda nyingine ya ujenzi wa masoko mawili. Tumamshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuipigania Arusha na kuiletea maendeleo makubwa kila kukicha,” amesema Gambo.

Leave A Reply