The House of Favourite Newspapers

WAZIRI MIFUGO AONYA UINGIZAJI MIFUGO KINYEMELA NCHINI

0
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza katika mkutano wake.
Mmoja wa Wafugaji akiuliza swali kwenye Mkutano huo

 

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amewatahadhalisha wafugaji waliopanga kuwadhuru wananchi waliotoa taarifa zilizosaidia Serikali kukamata mifugo iliyoingia nchini kinyume cha sheria hivi karibuni.

 

Ulega ametoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na wakazi wa kata za Mgagao na Kirya zilizopo wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro ambapo alisema serikali haitawavumilia watu wa aina hiyo na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vipo makini kuhakikisha usalama wa wananchi wa eneo hilo.

 

Alisema Serikali ipo makini na ina macho na masikio ya kutosha na ipo kila mahali na kwamba kama kuna mpango mbaya dhidi ya wananchi waliotoa taarifa hizo hautafanikiwa.

 

“Jambo limeshapita, acheni kutafuta mchawi. Mkae mkijua kwamba Serikali ina mkono mrefu, atakayethubutu kutenda mambo mabaya ataishia kwenye vyombo vya dola,” amesema Ulega.

 

Ulega alidai kupata taarifa za kuwapo kwa baadhi ya wafugaji kuanza vikao vya kuwatafuta watu waliotoa taarifa hizo.

 

Mbali na hilo, Ulega alisisitiza kuwa Serikali ya Rais Magufuli ipo makini na imelenga kuwatetea wanyonge na kwamba haina nia ya kuchukua mifugo ya wafugaji kwenye mchakato wa upigaji wa chapa.

 

Leave A Reply