The House of Favourite Newspapers

Serikali Yaweka Kitanzi Shoo Za Wasanii

0

Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’ kuruhusu shughuli mbalimbali ziendelee kama kawaida kuanzia Juni 29, mwaka huu, Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limeweka kitanzi kikali kwa wasanii watakaokwenda kinyume na maagizo ya Serikali, IJUMAA linakupa habari kamili.

 

Kauli hiyo ya Rais Magufuli ilikuja kufuatia kuwepo kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili kupita, Serikali ikiwa imezuia shughuli zote zinazohusisha mikusanyiko kutokana na tahadhari ya Ugonjwa wa COVID-19. Baada ya hali kutulia, Serikali imeruhusu wasanii kuendelea na kazi zao ikiwemo suala zima la kufanya shoo ila kwa kuzingatia masharti yaliyotolewa na Wizara ya Afya.

TUJIUNGE NA MNGEREZAA

kizungumza na Gazeti la IJUMAA kwenye mahojiano maalum (exclusive), Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza, alianza kwa kusisitiza tangazo la Rais Magufuli ambalo alilitoa Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akitoa hotuba ya kulivunja Bunge la 11.Mngereza alisema, tarehe rasmi ya wasanii kuanza kufanya shoo ni Juni 29, mwaka huu na kuna muongozo umetolewa, japo wapo ambao wanafanya kwa siri jambo ambalo ni kinyume na agizo.

 

KITANZI KIKALIA

lisema, wanaofanya shoo kabla ya siku hiyo, wakibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.“Tarehe rasmi ya wasanii kuanza kufanya shoo ni Juni 29, mwaka huu, lakini najua chini kwa chini wapo ambao wanaendelea, tukiwabaini tutawachukulia hatua.

 

WAMETOA MWONGOZO

“Kuna mwongozo ambao tumetoa kwa ajili ya masharti kuzingatiwa. Kimsingi, tulitoa mwongozo na umetokana na kikao cha Bodi ya Basata, kilichofanyika Mei 28, mwaka huu kwa ajili ya kuzungumzia namna ya kufanya kazi na kuchukua tahadhari.“Kwa sababu licha ya kwamba mheshimiwa Rais ameruhusu, bado masharti yanatakiwa kuzingatiwa juu ya maambukizi ya Virusi vya Corona.

WALIWASHIRIKISHA WADAU

“Hivyo katika kikao hicho tulivyokaa, tulipata mawazo mazuri kutoka kwa wadau wa sanaa, wasanii wenyewe, wamiliki wa bendi na wa kumbi za starehe.“Tulipata mawazo mazuri, ikiwemo washehereshaji (MC), ambao wana uwezo wa kucontrol watu, katika vipengele vyote, ambapo mawazo hayo yaliweza kutengeneza muongozo na mambo ya kuzingatia na tuliusambaza.

 

AWARUDIA WASANII

“Kwa upande wa wasanii na wadau wa sanaa, wanatakiwa kuzingatia na kuufuata muongozo huo katika shughuli zao.“Kama ukumbi una idadi ya watu 300, wanaweza wakaingia nusu yao, si lazima wote.

 

WASANII WANAUJUA

“Wasanii wanautambua mwongozo huo, wenye mawazo yao wenyewe katika vitu vya kuzingatia kwenye shoo zao,’’ alisema Mngereza.

MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO

Mbali na ishu ya shoo, Mngereza alizungumzia ishu ya wasanii wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii katika kufikisha kazi zao kwa mashabiki.Alisema kuwa, Baraza limekuwa likiwachukulia hatua kali wasanii wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii.

 

“Tumekuwa tukiwachukulia hatua kali wasanii wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii, hii ni kuwasaidia wasanii wenyewe.“Mbali na kutoa adhabu,balaza limekuwa likitoa semina kwa wasanii juu ya matumizi ya mitandao, tukishirikiana na wadau wetu ambao wana uelewa na kazi ya sanaa.

 

“Kwa sababu msanii akipata elimu juu ya mitandao, anakuwa na uelewa wa kazi yake, maana wapo ambao wamekuwa wakitumia kuposti picha za utupu ambazo hazina faida na kazi yake.

 

AGUSIA BAJETI

“Hata katika bajeti ya Julai, inaangalia ni kiasi gani inaweza kusaidia vijana katika matumizi ya mitandao,’’ alisema Mngereza.

 

ATOA RAI KWA WASANII

Mngereza alimalizia kwa kutoa rai kwa wasanii kujitambua na kufanya kazi kwa weledi.“Wasanii wanatakiwa wajue kwamba, nchi inajengwa na mazingira mazuri, hata katika hotuba ya mheshimiwa Rais, alisifia sana sekta ya sanaa.“Kwa mwaka 2018, sekta yetu ilipanda chati, ni eneo ambalo linazalisha ajira mbalimbali ikiwemo wasanii na sekta zingine za sanaa.

 

“Wasanii wanatakiwa wajue sanaa ni kazi kama kazi zingine, haiwezi kukosa muongozo na kanuni za kufuata.“Wasanii wana nafasi kubwa sana katika kuijenga jamii, waiheshimu kazi yao, maana wakitambua hakutakuwa na mivutano.“Milango ya Basata iko wazi, wanakaribishwa kushauriana nasi ili kuendelea kuleta maendeleo,’’ alisema Mngereza.

WASANII WANAONGOZA KWA SHOO

Miongoni mwa wasanii ambao watanufaika na kipyenga cha Juni 29 ni pamoja na C.E.O, wa Lebo ya King’s Music; Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, C.E.O wa Wasafi Classic Baby (WCB); Nasibu Abdul ‘Mondi’ na C.E.O wa Konde Gang Music Worldwide, Rajab Abdul ‘Harmonize’.Wengine ni Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Faustina Charles ‘Nandy’, Maua Sama, Juma Mussa ‘Jux’, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Yusuph Mbwana Kilungi ‘Mbosso’, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Hellen George ‘Ruby’, Abdul Iddi ‘Lava Lava’ na wengine.

CPWAA AMSHAURI VANESSA MDEE l MAPRODYUZA WAACHE KUIBA l NILIJUA SUMA LEE ATAOKOKA

Leave A Reply