The House of Favourite Newspapers

Seti ya kwanza ya treni ya kisasa ya EMU Yawasili katika Bandari ya Dar

0

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema Seti ya kwanza ya treni ya kisasa ya Electric Multiple Unit (EMU), vichwa vitano vya umeme na mabehewa matatu ya Abiria vimewasili katika Bandari ya Dar es Salaam

TRC imesema seti moja ina uwezo wa kubeba Abiria 589 na kutembea kwa kasi ya Kilomita 160 kwa saa na hadi sasa imepokea Mabehewa 65 ya Abiria, Vichwa 9 vya Umeme na Seti moja ya EMU huku seti nyingine zikiendelea kuwasili kila mwezi hadi Oktoba 2024

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Jamila Mbarouk amesema Maendeleo ya Mradi wa #SGR Awamu ya Kwanza yamefikia 98.90% kwa Dar- Morogoro (KM 300), Morogoro – Makutupora (96.51%), Makutupora – Tabora (13.98%), Tabora – Isaka (5.44%) na Mwanza – Isaka (54.01%)

Leave A Reply