The House of Favourite Newspapers

SGA Security Yawafunda Wahasibu Kuhusu Utunzaji wa Mazingira

0
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA), CPA Prof Sylvia Temu (wa pili kulia) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Tanzania CPA Eric Sambu baada ya kampuni hiyo ya ulinzi kutoa msaada wa miti kwa bodi hiyo ili ioteshwe kaika ukumbi wa mikutano wa APC, Bunju Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa SGA, CPA Jonathan Geleta na Mshauri wa NBAA CPA Simon Mponji.

 

 

KAMPUNI ya ulinzi ya SGA Security imetoa msaada wa miti kwa ukumbi wa mikutano wa APC uliopo Bunju Dar es Salaam na pia kuwafunda  namna ya utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti.

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA), CPA Prof Sylvia Temu (kushoto) akipokea zawadi ya mti kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Tanzania CPA Eric Sambu baada ya kampuni hiyo ya ulinzi kutoa msaada wa miti kwa bodi hiyo ili ioteshwe katika ukumbi wa mikutano wa APC, Bunju Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa SGA, CPA Jonathan Geleta.

 

 

Akizungumza katika mkutano wa mwaka wa wahasibu uliofanyika katika ukumbi huo wa APC, Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Tanzania, CPA Eric Sambu, ambaye alikuwa mmoja wa watoa mada katika mkutano huo, alitoa wito kwa wahasibu nchini kujenga utamaduni wa kupanda miti katika kila tukio  au sherehe.

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA), CPA Prof Sylvia Temu (wa pili kushoto) akizungumza baada ya kupokea zawadi ya miti kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Tanzania CPA Eric Sambu (kulia) wakati wa Mkutano Mkuu wa Wahasibu Jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa SGA, CPA Jonathan Geleta (kushoto) na Mshauri wa NBAA CPA Simon Mponji.

 

 

Aliwahamasisha kuhusu uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji wa miti huku akisisitiza kuwa kukata miti bila kuotesha mingine ina maana ukanda wote unaweza kugeuka kuwa jangwa kwa hivyo ni muhimu kila mmoja achukue jukumu la kuotesha miti na kuhamasisha jamii pia kuotesha miti kwa wingi.

 

 

“Kama kampuni inayotoa huduma za usalama na ulinzi, tunaamini utunzaji wa mazingira ni mwanzo wa maisha bora na hili lilisisitizwa katika mkutano wa COP 26 uliofanyika Scotland,” alisema.

 

 

Mkutano wa mwaka wa wahasibu huandaliwa na NBAA katika ukumbi wa APC kila mwaka na kuwaleta pamoja washiriki zaidi ya 3000 na hufanyika sambamba na tuzo za makampuni yaliyowasilisha mahesabu vizuri kwa mwaka husika.

 

 

kama ishara ya tuzo mbili walizopata mwaka huu katika tuzo za Tanzania Consumer Choices Africa, Bw Sambu alikabidhi miti miwili kwa Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA Prof. Sylvia Temu ili ioteshwe katika ukumbi wa APC.

 

 

SGA inafahamika kwa kutoa huduma za fedha, ulinzi, alarm, ulinzi wa kielektronia, na huduma nyingine na ilipigiwa kura kama kampuni bora ya ulinzi Tanzania na Afrika Mashariki. CPA Prof Temu, aliyechaguliwa katika nafasi hiyo kwa miaka mitatu, aliipongeza SGA kwa kuwakumbuka wahasibu na kuwahamasisha kuhusu mazingira.

 

 

Aliipongeza kampuni hiyo pia kwa mafanikio mbalimbali  pamoja na tuzo kwani inathibitisha imani ya watu kwa kampuni hiyo. Pamoja na tuzo mbili ilizopata, kampuni hiyo pia ilitambuliwa katika maonesho ya kimataifa ya madini yaliyofanyika Geita kama ishara ya ubunifu walioufanya katika ulinzi wa kielektronia kwa  migodi. SGA ndio ilikuwa kampuni  ya kwanza ya  binafsi ya ulinzi  ikijulikana kama Group Four Security.

Leave A Reply