The House of Favourite Newspapers

SHAMSA ATESWA NA WAPENZI WA ZAMANI WA MUMEWE

Shamsa Ford

STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford ameeleza kuteswa na wapenzi wa zamani wa mumewe, Chid Mapenzi ambapo kila kukicha wamekuwa wakimfanyia visa.  Akizungumza na Za Motomoto News, Shamsa alisema amekuwa akisumbuliwa na wanawake ambao waliwahi kutoka kimapenzi na mumewe ambapo kila anapokutana nao wamekuwa wakimfanyia visa kama kumpiga vikumbo na fujo nyingine za hapa na pale.

“Kiukweli wanawake wa zamani wa mume wangu wananisumbua sana, kila ninapokutana nao wananipiga vikumbo, wananifanyia visa na maneno kibao yakiwatoka huku wakitaja jina la Chid, naomba niwaambie tu kuwa wanatakiwa kukubaliana na hali halisi maana aliniona ninamfaa ndiyo akanioa na kuniweka ndani hivyo fujo wanazofanya hazisaidii bali wanatakiwa watafute wa kwao,” alisema Shamsa.

Stori: Gladness Mallya, Dar

Comments are closed.