The House of Favourite Newspapers

Shangwe la Harmonize Akiwasili Taifa Simba na Yanga – Video

0

WANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul Kahali maarufu Harmonize na Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’, juzi walikuwa sehemu ya watazamaji waliofika kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar kushuhudia mechi ya Yanga na Simba.

 

Wawili hao ambao walikuwa pamoja WCB kabla ya Harmonize kuondoka na kuanzisha lebo yake ya Konde Gang, wamekuwa washindani wakubwa kwenye soko la muziki hapa nchini.

 

Spoti Xtra lilianza kumshuhudia Diamond akifika uwanjani jana akiwa na mzazi mwenzake, Zari na watoto wao, Latiffah na Dylan wote walikuwa wamevaa jezi za Simba.

 

Baadaye ndipo akawasili Harmonize akiwa na walinzi wake, kisha wakati wa mapumziko, akaingia uwanjani kusalimia mashabiki ambao walilipuka kwa shangwe.Msafara wa Harmonize ulipata tafrani kidogo baada ya kwenda kukaa jukwaa la Yanga huku baadhi yao wakiwa na jezi za Simba ambapo walitakiwa kuondoka au kuvua ili wakae.

 

Waliovaa jezi za Simba ni Country Boy na Ibrah ambao walikubali kuvua na kukaa kushuhudia burudani iliyomalizika kwa sare ya 1-1.

Stori Na JMANJIRO LYIMO, NA LEEN ESSAU

Leave A Reply