The House of Favourite Newspapers

Shawn Mendes Avunja Ukimya, Ajibu Tuhuma za Ushoga

STAA wa Muziki duniani kutoka nchini Canada, Shawn Peter Raul Mendes maarufu kama Shawn Mendes  amefunguka kuhusu  tuhuma zinazomkabili za baadhi ya watu kumsema kwamba anashiriki mapenzi ya jinsia moja (shoga).

 

Kupitia mahojiano na Rollingston, Mendes  amesema kwamba maisha yake yamejawa na mambo mengi na uzito wa stress, “Napenda kusema sijali kuhusiana  na hilo lakini sio ukweli kwa haya mambo nimekuwa nikizushiwa kwa muda wa miaka mitano kuwa mimi ni shoga”.

 

Shawn Mendes ameeleza kwamba alipokuwa na umri mdogo alikuwa anaishi na binamu zake 15 wa kike, na alikuwa anasukwa nywele na kupakwa kucha rangi, kwa hiyo labda jambo hilo ndilo limesababisha watu wamuone kuwa ana muonekano kama mschana.

 

Mahusiano ya mwisho ya kimapenzi ya Mendes yalikuwa kati yake na Hailey Rhode Baldwin ambapo waliachana mwaka jana, na dada huyo akaingia kwenye mapenzi na staa wa Pop, Justin Bieber mpaka sasa.

MKWASA Ampa Somo Zito AMUNIKE Ataja FIGISU TAIFA STARS

Comments are closed.