The House of Favourite Newspapers

MTOTO WA CATHY AZUA MSHTUKO

Sabrina Rupia ‘Cathy’ na Mwanaye Issa Rupia

MTOTO wa msanii mkongwe wa filamu Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ anayejulikana kwa jina la Issa ameibua mshtuko baada ya kuonekana kwa mara ya kwanza huku akiwa ni kama kaka wa msanii huyo.

 

Kijana huyo aliibua mshtuko hivi karibuni baada ya mama yake  huyo kuanika picha wakiwa pamoja na watu kujiuliza Cathy alimzaa akiwa na umri gani.

Cathy aliiambia Za Motomoto News kuwa alimzaa mtoto wake huyo akiwa na miaka 16 hivyo hivi karibuni ndiyo yalikuwa mahafali yake ya kuhitimu digrii ya kwanza ndani ya Chuo Kikuu cha Sokoine, Morogoro.

 

“Huyu ni mtoto wangu wa kwanza, nilimpata nikiwa na miaka 16, namshukuru Mungu sikumdhuru kama mabinti wengi wanavyofanya wakipata mimba za utotoni, sasa nafurahia yaani ndiye huyu tumekua wote, nampenda sana, ni mwanangu, ni kaka yangu, ni mshauri wangu, kifupi ndiyo kila kitu kwangu,” alisema Cathy.

Stori: Gladness Mallya

Comments are closed.