The House of Favourite Newspapers

Shehe mkuu wa mkoa atahadharisha wafungaji

0

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa SalimNa Elvan Stambuli, Uwazi

DAR ES SALAAM: Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum (pichani) amewatahadharisha wafungaji wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kutorudia dhambi zao baada ya mfungo kwa sababu kufanya hivyo ni sawa na kumjaribu Mungu wakati hajaribiwi.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum, Shehe Mussa alisema ipo tabia ya Waislamu wakisha fungua Ramadhan, hawaswali tena na wanarudia vitendo ambavyo ni kinyume na mafundisho ya Mungu.

“Tumekuwa na miezi 11 ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakifanya dhambi lakini ametupa mwezi mmoja tu kutubu na ni Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, sasa inashangaza kuona watu badala ya kuendeleza yale mema waliyokuwa wakiyafanya, wanaacha na kujiingiza katika dhambi, hii ni hatari sana,” alisema.

Akifafanua zaidi kiongozi huyo alisema: “Wakati wa kufunga siyo tunajizuia tu kula ni kwamba masikio yanatakiwa yasisikie kitu kinachomuudhi Mungu, pua isinuse haramu, mfano manukato ambayo mwanamke anapaka ili kumshawishi mwanaume, mikono isiibe au kupiga au kupokea na kutoa rushwa, mdomo usinywe pombe au kuvuta sigara na kusema matusi, miguu isiende kunakokatazwa na dini na kadhalika.

“Haya mambo yanayokatazwa hata baada ya Ramadhan yanatakiwa yafuatwe kwani Ramadhan ni darasa na tuliyojifunza yanatakiwa kuendelezwa.”

Soma mahojiano kamili katika gazeti hili toleo lijalo Jumanne.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply