The House of Favourite Newspapers

Shoga; Siyo mpaka akuanze yeye

0

Couple-in-BedNimshukuru Mwenyezi Mungu kwa upendo wake wa dhati kwa kunifanya nipate kibali cha kuandika makala haya.

Niwatakie mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ndugu zangu Waislamu wote nchini na duniani kwa ujumla ikiwa leo ni siku ya 6 ingawa wengine ni tofauti.

Nianze kwa kujikita kwenye mada yangu ya leo ambayo kwa waelewa itawatoa tongotongo wanawake ambao siku zote wamekuwa nazo kwenye uhusiano wao kwamba kama mume wake asipomuanza kwa chochote basi yeye hawezi kuanza.

Wapenzi kulalamikiana

Kama huko hivyo hilo ni tatizo, tena tatizo kubwa sana ambalo wanawake hasa walio kwenye ndoa linasababisha wawe watu wa kulalamika.

Kila kitu aanzwe

Kilichopo mwanamke anataka ukiamka uanze kumsalimia, ukiondoka nyumbani uanze kumwambia kuwa umefika ofisini salama, ikifika muda wa chakula (Lunch time) pia uumuulize. Hivi baby umekula, hata muda wa chakula cha usiku ukifika anataka uanze kumuandaa wewe. Ukisafiri kadhalika anataka wewe ndiye uwe wa kwanza kumjulia hali, kweli!

Jukumu la wote

Suala la kutuma ujumbe, kumpiga simu au mawasilino ya aina yoyote yale kwa wanandoa ni jukumu la wote na kama utakuwa unasubiri kila siku uanzwe wewe tu, si sawa, unakosea na kumbebesha lawama mwenzio.

Wanawake wengi wamegeuka walalamikaji pasipo kujifanyia tathmini kuwa wao ndiyo chanzo na wala suala hilo halipaswi kumlalamikia shoga yako kuwa huanzwi, si uanze.

Usiishi kwa mazoea

Acha kuishi kwa mazoea kwamba mwanaume ndiye anapaswa kuwa mwanzilishi wa kila kitu, ingawa kiasili ndivyo ilivyo lakini kama ukiona hajakuanza inawezekana hayuko kwenye ‘mudi’ wakati mwingine kachoka, cha kufanya ni wewe kumwambia mume wangu nakuhitaji  na maneno mengine kama hayo yenye kuashiria uhitaji wa faragha.

Si umuanze na wewe

Hivi jamani kama mpenzi wako hakupigii simu, hachati na wewe Facebook, WhatsApp au mtandao wowote ule ndiyo chanzo cha kusema kuwa hakupendi na hakujali, kama ndiyo kwa nini wewe hujamtaka mchati naye, basi na wewe humpendi.

Mpenzi msomaji, mapenzi hayataki hivyo kama unahisi una hamu ya kukutana na mwenzio tafadhali fanya hivyo, mwambie “baby nina hamu na wewe, napenda leo tuwe sote, nahisi kuwa karibu nawe, natamani unikumbatie nipate joto lako zuri, nililolimisi muda mrefu, siyo kusubiri akuanze.

Mapenzi siyo msaafu kwamba lazima uwe vile vile siku zote ukifikiria hivyo unakuwa unakosea sana, mapenzi yanahitaji ushirikiano, mapenzi yanahitaji maelewano kabla na baada ya tendo husika.

JIREKEBISHE!

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply