The House of Favourite Newspapers

Sherehe ya Ndoa: Bw., Bi Harusi Watua na Helikopta Ukumbini

0

JAMAA mmoja aliyefahamika kwa jina la William Moye mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro ameweka rekodi ya aina yake baada ya kuwafanyia sapraizi mashuhuda na ndugu waliohudhuria kwenye harusi yake.

 

Katika sherehe hiyo iliyofanyika hivi karibuni, Moye alingia ukumbini akiwa ndani ya helikopta na mkewe ambapo  wengi walishangaa na kupiga makelele ya shangwe kwa furaha kwa kuwa hawakutarajia kitu hicho kutokea.

 

 

Moye na mkewe wamesema walifanya hivyo kwa sababu harusi ni kitu cha mara moja, hivyo watu wakipata fursa wasihofie kutumia pesa ili iwe ya harusi ya nguvu.

 

“Sisi tunaamini tutadumu kwenye ndoa yetu licha ya imani zilizojengeka vichwani mwa baadhi ya watu kuwa waliotumia gharama kubwa huwa hawadumu,” alisema Moye.

Leave A Reply