The House of Favourite Newspapers

Sherehe ya Shilole Yasengenywa

Mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mume wake Ashrafu Uchebe.

 

LICHA ya mbwembwe nyingi kwenye sherehe ya harusi ya Mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’ iliyofanyika wikiendi iliyopita kwenye Ukumbi wa Hekima Garden, Mikocheni ambapo alimwagiwa minoti kibao, baadhi ya wageni waalikwa walijikuta wakiondoka na dukuduku na kuisengenya shughuli hiyo kutokana na kukosa msosi.
Chanzo makini kilichokuwa kwenye sherehe hiyo kilinyetisha kuwa, licha ya ishu hiyo iliyohudhuriwa na mastaa mbalimbali kufana vilivyo, tatizo kubwa lilikuwa kwenye chakula, kwani baadhi ya wahudhuriaji walijikuta wakiishia kwenye foleni msosi ukawa umeisha.

Wakifanya yao.

 

Mikito Nusunusu ilimwendea hewani mume wa Shilole, Ashrafu Uchebe baada ya kupata ubuyu huo ili aeleze kilichotokea naye alikuwa na haya ya kusema;

“Binadamu hawana jema, hata uwafanyie nini hawatakosa cha kuongea hivyo hizo ni hila za binadamu, kikubwa tunamshukuru Mungu shughuli yetu ilienda vizuri.”

Comments are closed.