The House of Favourite Newspapers

SHIGONGO Awapa Somo Wanafunzi IFM Wainama Vichwa Chini!! (Picha +Video)

MKURUGENZI Mtendaji wa Makampuni ya Global Group na Mhamasishaji Maarufu Afrika Mashariki na Kati, Eric Shigongo  jana amewaasa wanachuo waliohudhuria Kongamano la The Life Definition 2019  kuhakikisha wanabuni mbinu mbalimbali za kujikamua na kufikia malengo yao,  huku akiwaasa kutumia taaluma waliyonayo kujiajiri na kufungua njia kwa watu wengine ili waweze kuyafikia malengo yao.

Mkuruenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo (kusoto) akizungumza na wanachuo Cha IFM jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la The Life Definition 2019  jana.

Akizungumza kwenye Kongamano hilo lililofanyika katika Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam Shigongo aliwataka vijana hao kujitoa kwa nguvu zao zote ili kufanikiwa na kutimiza ndoto zao zaidi akiwahamasisha kuwa macho kwa kuwa mtaani bado kuna fursa nyingi ambazo zinahitaji watu kuzitengeneza na kuziendeleza kwa manufaa ya jamii inayaowazunguka.

Shigongo (kulia) akizungumza na wanachuo Cha  Cha Usimamzi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la The Life Definition 2019.

Shigongo alisema, changamoto katika maisha ndiyo iwe suluhisho la mafanikio yao, hivyo watumie nafasi hizo kama fursa ya kutatua changamoto na mwisho wake yawaletee mafanikio ambayo watu wengi hasa vijana wamekuwa wakiyaota kila siku.

Mkurugenzi huyo aliwataka wanachuo hao kuondokana na dhana ya kujidharau, kuangalia familia walizotoka na kwamba hata kama wametoka familia maskini lakini wanaweza kutoka hapo walipo na kuzikwamua familia zao kama ambavyo yeye aliamua kuchukua uamuzi wa kuukataa umaskini na kuzivaa changamoto za maisha na hatimaye alizishinda na ndiyo maana leo amepata mafanikio.

Lakini pia alitumia njia ya mifano katika kufikisha ujumbe wake, ambapo alimtolea mfano

Emmanuel Mathias ‘MC Pilipilia’ akiwapa historia ya maisha yake hadi kufikia hapo alipo hivi sasa. 
Msanii wa Bongo Fleva Menina naye alikuwa miongoni mwa wazungumzaji katika kongamano hilo.
Muigizaji  aliyejipatia Umaarufu mkubwa kupitia Tamthilia ya Mahusiano Mwinjaku akizungumza na wanachuo waliohudhuria hafla hiyo ya kuwapa mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto katika maisha ya chuo na hata watakapomaliza.
Mchekeshaji kutoka kundi la Timamu Mr. Beneficial akizungumza mambo mbalimbali juu ya kujikwamua kimaisha.

 

Babu wa Loliondo aliyegundua fursa ya uhitaji wa tiba fulani kwenye jamii na hatimaye alitumia mwanya huo kujipatia mafanikio na kutimiza ndoto zake.

 

Ambapo pia aliwataka vijana hao kutumia muda wao vizuri na kuachana na masula mengi ambayo yanakuwa hayana msingi na faida katika maisha yao ya kila siku.

Comments are closed.