The House of Favourite Newspapers

Shilole Atokwa na Machozi Kisa Tuzo ya Aunt Ezekiel

Zuwena Mohamed ‘Shilole’

 

SIKU chache baada ya msanii wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel kumtunuku Tuzo ya Mama Bora ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amepokea tuzo hiyo kwa msisimko hadi kutokwa na machozi.

Akizungumza na Showbiz, Aunty alisema ameamua kumpatia zawadi hiyo siku ambayo alikuwa akizindua filamu yake ya Mama kutokana na Shilole kuwa ni mama bora ambaye siku zote amekuwa akitafuta pesa kwa shida ili wanaye wasome vizuri.

“Kwenye siku hii muhimu nikaona itakuwa sio jambo baya kama mimi na timu yangu nzima nikamzawadia huyu mtu (Shilole), sijui niseme tuzo ya mama bora au zawadi ya mama bora, kwasababu kwa upande wangu yeye ni mama bora, ni mtu ambaye anatafuta sana, anafanya kazi kwa shida sana ili watoto wake wasome kwenye shule za gharama na mtu huyo ni Shilole,”alisema Aunt

Showbiz ilimtafuta Shilole ili kutaka kujua kwa upande wake amelipokeaje hili, ambapo alijibu; “Nilikuwa shocked kuona Aunty Ezekiel kanichagua kuwa mama bora, nililia kwa furaha kuona pia msanii mwenzangu ameweza kunitunuku, namshukuru sana, na hii imenipa nguvu ya kuendelea kufanya kazi kwa nguvu zangu zo

Comments are closed.