The House of Favourite Newspapers

Shilole Ubonge Umembadili Jina

Chibonge! Staa wa filamu na Bongo Fleva ambaye pia ni mpishi wa madikodiko, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amesema ubonge umemfanya abadilishiwe jina na kuitwa mjamzito.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Shilole au Shishi Baby alisema alishaanza kuchoka kuambiwa ni mjamzito wakati hana hata dalili hivyo amegundua jambo la kufanya ni kuacha uvivu na kuingia ‘gym’ ili kupunguza mwili.

 

“Unajua inakera, mtu huna hata mpango wa kuzaa halafu unaulizwa

una mimba ya miezi mingapi? Lazima mtu uchanganyikiwe. Hapa nimeanza kampeni ya kurudisha mwili wangu kwa kasi kubwa,” alisema Shilole au Shishi Trump.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Comments are closed.