The House of Favourite Newspapers

Shirika la Umoja wa Mataifa la UNFPA, CCBRT na AMREF Kuadhimisha siku ya kutokomeza Fistula duniani

0
Mkurugenzi Mkazi wa UNFPA –Tanzania, Dr. Hashina Begum akizungumza na wanahabari.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Tawi la Tanzania kwa kushirikiana na CCBRT na AMREF  wanatarajiwa kuadhimisha kilele cha siku ya kutokomeza fistula duniani Mei 23, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mwakilishi mkurugenzi mkazi wa UNFPA –Tanzania, Dr. Hashina Begum amesema kuwa tatizo la Fistula ya uzazi kwa nchi zilizoendelea lilishatokomezwa ukilinganisha na nchi zinazoendelea ambapo wanawake wengi wamekuwa wakikabiliwa na aibu na kupoteza matumaini ya maisha na kusema kuwa ni jukumu la vyombo vya habari nchini kushirikisha jamii ili watu wote waelimike.
Amesema kuwa Fistula inatibika bure na ni muda muafaka wa kurudisha tumaini, heshima na uponyaji kwa wote waliokumbwa na tatizo hilo.
Naye meneja mradi wa Fistula kutoka Hospitali ya CCBRT, Clement Ndalimi akizungumza kwa niaba ya afisa mtendaji mkuu wa CCBRT, amesema kuwa zaidi ya wanawake 15,000 hukumbwa na tatizo la Fistula ambapo wanawake 4,000 mpaka sasa wametibiwa ugonjwa huo.
Ameongeza kuwa, ili kutokomeza tatizo hilo ni muhimu kwa mama mjamzito kuwahi mapema kliniki pindi anapogundua kuwa ni mjamzito ili kuepukana na Fistula.
Amebainisha kuwa, imani potofu kwa jamii ya kwamba Fistula haitibiki si kweli bali pia ni vyema kuzingatia kujiepusha na mimba za utotoni ambazo zimekuwa tatizo kubwa linalosababisha vifo vya mama na mtoto pamoja na Fistula ya uzazi.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa AMREF Tanzania, Bi. Florence Temu amesema mama anayejifungua anahitaji kupata huduma bure na kubainisha kuwa asilimia 25 tu ya wajawazito wanaowahi mapema vituo vya afya kwa ajili ya uangalizi wa awali.

Na DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply