The House of Favourite Newspapers

Shirikisho la Filamu Tanzania kufanya uchaguzi Alhamisi

0

1.Kutoka kushoto ni Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ,Francis Kaswahili,Mwenyekiti wa Kamati huru ya Uchaguzi ,Methew Bicco na Makamu Mwenyekiti Kamati ya Ucaguzi,Shamsa Danga. Kutoka kushoto ni Katibu wa Kamati ya Uchaguzi, Francis Kaswahili, Mwenyekiti wa Kamati huru ya Uchaguzi, Methew Bicco na Makamu Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi, Shamsa Danga.

2.Viongozi hao wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).
Viongozi hao wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).

3.Wanahabri wakifuatilia mkutano huo.
Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

KAMATI ya Uchaguzi ya Bodi ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) imetangaza siku ya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa ngazi za rais, makamu na wajumbe.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa kamati hiyo, Methew Bicco amesema kuwa tayari kamati imeshapitia majina ya wagombea na kujiridhisha kuwa wana vigezo na wana haki ya kushiriki katika uchaguzi huo utakaofanyika ndani ya Ukumbi wa Urafiki, Ubungo jijini Dar.

Bicco amewataja watu wawili ambao kamati imewapendekeza kuingia katika kinyang’anyiro cha nafasi ya urais kuwa ni Simon Mwakifwamba na Issa Kipemba ambao tayari wameshaanza kampeni hadi Februari 24, 2016.

Kwa upande wa Makamu wa Rais, Bicco alisema jina moja la Deosonga Njelekela ndilo lililopatikana kwani hakukuwa na majina mengine yaliyowania nafasi hiyo, hivyo litapigiwa kura jina hilo.

Kwa upande wa wajumbe wa bodi majina yaliyopatikana kuwania nafasi hiyo ni Ummy Mohamed Mpallu, John Justine, Daniel Basila, Irene Sanga, Mwanaharusi Ibrahim, Ally Mohamed (Baucha), Hussein Athuman, William Mtitu, Single Mtambalike, Michael Deodatus, Juma Issa Chikoka, Adamu Mikidadi na Abdulazizi Salehe Babuu ambapo majina yanayotakiwa kuunda kamati ni tisa tu.

Bicco aliongeza kuwa, mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, rais ambaye atakuwa amepatikana wa Shirikisho la Filamu Tanzania kwa mujibu na taratibu za bodi atatakiwa kuwachagua wajumbe wawili ili kuongeza idadi ya wajumbe tisa watakaokuwa wamechaguliwa.

(NA DENIS MTIMA/GPL)

Leave A Reply