The House of Favourite Newspapers

SHISHI ATOA SIRI YA KUMGEUZA UCHEBE ‘VIDEO KING’

Zuwena Mohammed ‘Shilole’ na Mumewe, Ashrafu Uchebe

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ametoboa siri ya kumgeuza mumewe, Ashrafu Uchebe kama ‘Video King’ kwenye wimbo wake wa Mchaka Mchaka kuwa ni kutokana na wivu alionao mwanaume huyo.  Akipiga stori na Mikito Nusu Nusu, Shilole alisema kuwa, mumewe huyo huwa hapendi sana kumuona akishuti video na wanaume huku ‘akibambiwabambiwa’ hivyo ili kumfanya awe na amani ndipo akamtumia yeye kwenye video hiyo.

“Ule wimbo kwanza nilimuimbia yeye, lakini Uchebe ana wivu sana, huwa hapendi kuona nashikwashikwa na wanaume kwenye video au hata kwenye steji, ndiyo maana nikaona kwa wimbo huu ambao nimemuimbia, siyo vibaya nikamtumia na kakinogesha kichupa ile mbaya,” alisema Shilole.

STORI: Hamida Hassan

Comments are closed.