Shoga: Shtuka! Ukizubaa Utaachiwa Mkia

 

HALOOO eeehhh tena ya kisoda! Anti Naa mwenyewe nimekuja tena na safari hii nipo kuwatetea wanawake wenzangu, shtuka shoga yangu vinginevyo mtakalia vimaneno vya kijinga wakati nyumba inateketea. Sipendi jamani mbona hivyo!

Hivi sisi wanawake nani katuroga? Inafika mahali tunajitoa akili wakati tunazo! Kuna mwanaume mmoja analalamika eti kutoswa na mpenzi wake ambaye alijichinjia mwenyewe na kuamini ng’ombe mzima atakula mwenyewe, lakini maskini mwisho wa siku kaachiwa mkia tu, ng’ombe wote wamekula wengine, alichoambulia kuchinja tu! Heee heee heeeiyaaaa!

Jamani ninaozungumza nao ni watu wazima waliovuka miaka 18 mbona mnanitolea mimacho kuonesha bado hamjanielewa namaanisha nini? Jamani kuchinja ng’ombe ni kuondoa usichana wa mwanamke kwani kisu kikishapita kuliwa ni halali na mkia ni ndoa, upo? Siyo unanitolea mijicho kama unasubiri meseji ya pesa umeahidiwa kutumiwa mwisho wa siku kila meseji unaona ni pesa hata ya tafadhali nipigie!

Baba wa watu baada ya kujichinjia aliamini kabisa yule mwanamke sasa ndiye wa kufa na kuzikana, lakini wajanja wakamuonjesha utamu na kumuachia mkia akibakia akilalama.

Shosti wangu ninaposema haya yanatoka moyoni, na si yeye tu, kina baba wengi huamini kumtoa mwanamke usichana wake, basi unakuwa umemaliza kila kitu. Jamani kuchinja ni sifa tu lakini ujuzi ndiyo kinga ya uhusiano wako, upo babu weee!

Si kila mchinjaji hula mapaja na mbavu wapo wanaochinja bila kula na mla mapaja na mbavu akawa mtu mwingine kabisa tofauti na mchinjaji. Lakini naamini wapo wanaume wanaamini akishamtoa mwanamke usichana basi ndiye lazima atakuwa mkewe, wanasahau kuna watu ndiyo mchezo wao kukata kichwa na kumuachia mkia uliwe na mwingine.

Mapenzi ya mwanamke ambaye hajaolewa hayatokani na kukatwa

kichwa bali mapenzi ya dhati. Wanawake wengine si waaminifu kwa asili hata ukimkata kichwa bado atapapatika na kwenda kuangukia kwa mtu mwingine kwa vile tu alikuwa na wewe kwa sababu ya kitu f’lan, hilo nalo neeeno!

Siku hizi kumkuta msichana na shingo yake

(usichana) ni adimu kama kutumiwa meseji ya pesa kwa bahati mbaya. Hivyo basi kuitoa kwa chipsi yai haoni shida kwa vile zama za ndoa kupata sifa kwa ajili ya kumkuta msichana hajamjua mwanaume wake wengi wanaona imepitwa na wakati.

Jamani si kwamba nawatetea wanawake wapoteze usichana wao la hasha, sisi enzi zetu msichana aliyeolewa bila usichana alikuwa hana thamani lakini siku hizi imebadilika watu hawaamini msichana leo kuolewa akiwa na usichana tofauti na zamani watu walikuwa wanashtuka kusikia hana.

Lakini bado nasisitiza shtuka, ng’ombe uliyemchinja si wa kumuacha mbali, ukizubaa utaachiwa mkia. Kama hujanisoma unaweza kunitumia meseji tu kwa namba yangu hapo juu.

Ni mimi Anti Naa wa Ukwee au ukipenda Shangingi Mstaafu!

Breaking News: Jambazi Aliyeongoza Mauaji ya Polisi 8 Kibiti Auawa -Dar


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment