Sholo Aomba Radhi, Aahidi Makubwa Pasaka

Sholo Mwamba.

 

KUFUATIA kuingia mitini katika tamasha la Mwaka Mpya, Mkali wa Singeli, Sholo Mwamba ameweka wazi kuwa kilichotokea ni kwamba aliponzwa na tamaa baada ya kupata dili lingine hivyo anawaomba radhi mashabiki wake huku akiahidi makubwa kwenye shoo ijayo.

 

Mkali huyo ni miongoni mwa mastaa wakubwa wa mziki huo watakaopanda kwenye steji moja na wakali wengine ambao ni Man Fongo na Dulla Makabila katika pambano hilo la Usiku wa Mwisho wa Ubishi litakalofanyika Aprili Mosi, mwaka huu (Sikukuu ya Pasaka) kwenye Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, Dar.

 

Akizungumza na Over Ze Weekend, Sholo Mwamba alisema kuwa, Watanzania kwa jumla wanapaswa kutambua kwamba wanaofanya muziki huo wametoka kwenye maisha ya kawaida hivyo wakati mwingine hupatwa na tamaa kutokana na ofa nyingine za kazi wanazopokea.

Man Fongo.

“Kwanza Watanzania wanatakiwa waelewe sisi tunaofanya mziki huu

tume-tokea uswahilini na bado tunaw-aomba waen-delee kutusapoti, ni kweli shoo ambayo ilitakiwa kufanyika sehemu ya Mbagala nikawa sijafika kutokana na mambo ambayo siwezi kuyaficha kwa kuwa bado nataka kutengenza muziki wangu.

 

“Huenda ikawa ni kawaida kwa vitu ambavyo vinatokea wakati wa sikukuu, unaweza mtu akaja akakupa kazi, lakini kesho yake anakuja mwingine anakupa kubwa zaidi ya ile awali na ukiangalia bado nahitaji ili nifikie malengo yangu, hii ilitokea kwa mashabaki wangu wa Dar live kwa kuwa niliponzwa na tamaa kijana wao naomba wanisamehe.

 

“Nimejifunza kwa kilichotokea, nawaomba mashabiki wangu waje kwa wingi Siku ya Pasaka waone nilichowaandalia,” alisema Sholo Mwamba.

Makabila.

Kwa upande wa mratibu wa shoo hiyo ambaye ni meneja wa Dar Live, Rajab Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa, mbali na mchuano huo, pia kutakuwa na vita nyingine ya wakali wa Taarab kati ya Jahazi Modern na Yah TMK.

 

KP aliongeza kuwa, kiingilio katika shoo hiyo ya aina yake kitakuwa ni buku saba yaani shilingi 7,000 huku michezo mbalimbali ya watoto ikiwemo kuogelea itafanyika kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi 12:00 jioni kwa mtonyo wa buku tatu tu.

OVER ZE WEEKEND


Loading...

Toa comment