The House of Favourite Newspapers

SHOO YA JIDE MLIMANI CITY HATAREE…!!!

Lady Jaydee

MWANAMUZIKI nyota wa kizazi kipya nchini, Lady Jaydee,  usiku wa kuamkia leo aliangusha bonge la shoo iliyokwenda kwa jina la Vocalo  ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar. Katika shoo hiyo alisindikizwa na wasanii mbalimbali akiwemo AY, MwanaFA na Ben Paul,  na kutoka nje ya nchi alikuwemo mwanamuziki maarufu wa Uganda, Juliana Kanyomozi,  na Zahara kutoka Afrika Kusini. Shoo hiyo ilikuwa hatareee…

Matukio katika picha:

       Mwanasiasa mkongwe nchini, John Momose Cheyo,  na kampani yake walivyowasili ukumbini.

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza (kulia) akimsikiliza kiumakini Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mungereza.AY naye alipanda jukwaani kutoa sapoti.

MwanaFA akikamua.

Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, akimpongeza AY kwa kazi nzuri aliyoifanya jukwaani.

Jide  (kulia) akisalimia mashabiki.

Mwanamuziki Zahara kutoka Afrika Kusini (kulia) akitoa burudani sambamba na mashabiki wake.

Shabiki akimkumbatia Zahara kimtindo baada ya kumnogesha kwa makamuzi yake.

Baadhi ya mashabiki walikosa viti na kushuhudia shoo wakiwa wamesimama kama hawa.

PICHA: RICHARD BUKOS/GPL        

Comments are closed.