The House of Favourite Newspapers

Shuhudia Haji Manara Alichomfanyika Shabiki wa Yanga (Video)

0

Katika kuelekea mchezo wa leo Jumatano, Agosti 23 wa watani wa jadi katika Dimba la Taifa, Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara amemfanyia kitu mbaya shabiki wa Klabu ya Yanga baada ya kumuekesha jezi ya klabu hiyo chini na kumpa kiasi cha fedha shilingi 10,000.

Homa ya mchezo huo umepanda kila kona ya Jiji la Dar, huku mashabiki wa pande zote wakitamba kuwa timu yao itaibuka na ushindi. Hii ni kutokana na upinzani mkubwa ambao umekuwepo kwa zaidi ya karne moja sasa.

Yanga wakiwa na Ibrahim Ajibu waliyemsajili kutoka Simba, wanatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Simba ambao wamemnyakua Niyonzima kutoka Simba. Mwamuzi ni dakika 90, tusubili kuona kama Yanga au Simba atakayeibuka kidedea kwenye mtanange huo.

MSHUHUDIE MANARA AKIMFANYIA KITU MBAYA SHABIKI WA YANGA

Leave A Reply