The House of Favourite Newspapers

Si Kweli Kwamba Kinyonga Huwa Anapasuka Ili Kuzaa

 WIKI hii kwenye Ndondoo za Mnyama ninamzungumzia kinyonga ambaye wengi wanamfahamu kutokana na sifa yake ya kubadilikabadilika rangi na mwendo wa taratibu.

 

Kila mtu huwa anamtazamo wake kuhusu kubadilika rangi kwa kinyonga wengine wakimuhusisha na mambo ya kishirikina, kuzuia mvua, kumfanya mjamzito asizae endapo atamshika huku wengine wakisema kinyonga mwenye mimba huwa hazai bali hupasuka na watoto kutoka kwenye tumbo huku mama yao akiwa amekufa. Makala haya yatakujuza zaidi.

Kinyonga ni mnyama ambaye yuko kwenye kundi la wanyama aina ya mjusi, kenge, mamba na wengineo.

Maajabu ya kinyonga ni kuweza kuzungusha macho yake kwa kipenyo cha nyuzi 360 huku kila jicho anaweza kulizungusha kwa uelekeo wake tofauti na ana uwezo wa kuona taswira mbili tofauti. Uzito wa kinyonga huanzia kati ya gramu 60 hadi gramu 180.

 

Kinyonga hubadilisha rangi kutokana na mazingira aidha ya hisia za mwanga au joto, baridi, njaa au hofu ya adui na mazingira hatarishi kwake. Hubadilisha rangi hiyo anapokuwa anapeleka taarifa kwenye ubongo wake.

Tofauti na wengi wanavyodhani kuwa huwa anabadilika ili kujificha anapoona aduzi zake.

 

Vinyonga wako zaidi ya aina mia moja, wamegawanyika katika makundi matatu, kundi la kwanza linajulikana kama Veiled chameleon, anakuwa na urefu wa sentimita 35 hadi 45 na anaweza kuishi kwa miaka mitano.

 

Panther chameleon huwa na urefu wa sentimita 43 na anaweza kuishi miaka miwili hadi mitatu na Jackson’s chameleon huwa na urefu wa sentimita 23 hadi 33 na anaweza kuishi kwa miaka mitano hadi 10.

 

Mara nyingi kinyonga hubadilika kutoka kwenye rangi ya kahawia kwenda kijani na hudhurungi, madoa madoa na kurudia hali yake ya awali lakini wanaweza kubadilika pia kwenye rangi zingine, kitendo hicho huchukua sekunde 20.

 

Nusu ya aina ya vinyonga wote duniani wanapatikana katika Kisiwa cha Madagascar na kuna zaidi ya aina 150 za vinyonga duniani lakini aina 59 zinapatikana kisiwani humo.

Itaendelea wiki ijayo.

DONDOO ZA WANYAMA | UWAZI

Comments are closed.