The House of Favourite Newspapers

Sikukuu ya Pasaka: Kanisa la VCCT Lililopo Mbezi Dar, Limeandaa Tamasha Kubwa

0

Kuelekea Sikukuu ya Pasaka, Kanisa la VCCT lililopo Mbezi jijini Dar es Salaam, limeandaa tamasha kubwa la Easter Production 2022 ‘A Thousand Reasons’ litakalojumuisha maonesho ya jukwaani ya tukio zima la kuteswa hadi kufufuka kwa Yesu Kristo pamoja na maigizo ya maisha ya Yesu kama angeishi kwenye kizazi cha sasa na mambo mengine mengi ya kusisimua.

Tamasha hilo litafanyika kwa siku tatu mfululizo, Ijumaa Kuu, Jumamosi ya Pasaka na Jumatatu ya Pasaka ambapo kutakuwa na viingilio vya shilingi 50,000 kwa package ya Golgotha, shilingi 30, 000 kwa package ya Gethsemane na shilingi 10,000 kwa package ya Desciples huku watoto wakiingia kwa shilingi 5,000 tu.

Milango itafunguliwa kuanzia saa 11 jioni na unaweza kulipia kupitia App ya Nilipe au fika VCCT Mbezi Beach au unaweza kupiga simu namba 0762441719.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave A Reply