The House of Favourite Newspapers

Silinde: Kwa Nini BOMBARDIER Kuliko Maji kwa Wananchi? – Video

Mbunge wa Momba, David Silinde (Chadema), amesema badala ya serika kutumia fedha nyingi kununua ndege kwa nini fedha hizo zisielekezwe katika miradi ya maji sehemu mbalimbali nchini.

 

Silinde amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo wakati akiuliza swali la nyongeza ambapo amesema maji yanayotumiwa katika vyoo maeneo ya mijini yanaonekana ni safi kuliko maji yanayotumiwa kwa matumizi ya nyumbani katika maeneo ya vijijini.

 

Katika swali lake msingi, Silinde alihoji “tatizo la maji Momba halijapatiwa ufumbuzi wa kudumu hadi sasa, je serikali itamaliza tatizo hilo Wilaya ya Momba,”

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesema kwa kiasi kikubwa tatizo la maji limetatuliwa sehemu nyingi nchini na pia ndege ina umuhimu wake.

 

“Mheshimiwa Mwenyekiti naomba nimwambie mbunge kuwa serikali inatambua tatizo la maji katika Wilaya ya Momba ambapo katika utekelezaji wa Awamu ya Kwanza ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP), seikali pia imekamilisha ujenzi wa vijiji vya Namtambala, Iyendwe, Itumbula, Mnyuzi, Chilulumo na Kamsamba katika jimbo la Momba.

 

“Pia serikali imetenga Sh bilioni moja katika jimbo hilo lakini pia kwa kuwa kazi ya Mbunge ni kusimamia, nitaomba asimamie fedha hizo zitumike vizuri katika mradi kusudiwa,” amesema Aweso.

 

Comments are closed.