The House of Favourite Newspapers

SIMANZI NA MAJOZI, ISAAC GAMBA AZIKWA BUNDA

SIMANZI NA MAJONZI vimetawala wakati mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW) nchini Ujerumani, Isaac Muyenjwa Gamba ukizikwa kwenye makaburi ya familia yao yaliyopo Kijiji cha Wanyere, leo Jumatano, Oktoba 31, 2018, Bunda mkoani Mara.

Gamba amezikwa baada ya ibada maalum ya kuaga mwili wake iliyofanyika nyumbani kwao Bunda Mjini na kuongozwa na Kwaya ya Waadventista Wasabato (SDA) kisha kupelekwa kwenye makaburi hayo ambayo yapo nje kidogo ya mji huo. 

Mamia ya waombolezaji wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, Katibu Mkuu wa Chadema -Zanzibar, Salum Mwalimu na wengine wamejitokeza na kuungana na wanafamilia pamoja na waombolezaji kuzika mwili wa mkongwe huyo katika tasnia ya habari.

Akizungumzia msiba wa Gamba, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili amesma kuwa kifo cha hicho kiwe funzo kwa Watanzania waishio ughaibuni kuwa wanapaswa kuiga mfano wake wa yale aliyoyafanya akiwa nchini ujerumani ya kuhabarisha umma kuendana na taaruma yake.

Aidha, Bupilipili ameushukuru uongozi wote wa DW kwa kufanikisha shughuli zote za kuuleta mwili wa marehemu hadi kufika mjini Bunda na watu wote waliohakikisha mwili huo unafika salaama na kuwafariji familia.

Gamba alikutwa akiwa amefariki chumbani kwake Alhamisi, Oktoba 18, mwaka huu, jijini Bonn nchini Ujerumani alikokuwa akifanya kazi zake.

Baada ya uchunguzi wa hospitali nchini Ujerumani, imegundulika kuwa kilichosababisha kifo chake ni kuvuja kwa damu kwenye ubongo (Brain Hemorrhage) yaani presha ya damu.

 

PICHA NA DENIS MTIMA | GPL

Kauli ya Mwisho ya Gamba kwa Mama Yake Mzazi

Comments are closed.