SIMBA KUCHEZA MECHI YAO SAA 9 ZAMBIA

Wachezaji wa timu ya Simba wakifanya mazoezi mjini Kitwe, Zambia.

MECHI ya Nkana na Simba kwenye hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa itachezwa saa 9 alasiri mjini Kitwe, Zambia umbali wa saa 2 kutoka jijini Lusaka, makao makuu ya nchi.

 

Muda huo itakuwa ni saa 10:00 jioni kwa saa za Tanzania kwani Kitwe wako nyuma saa moja ukilinganisha na Dar es Salaam. Simba ilifuzu hapo baada ya kuwaondosha Mbabane Swallows kwa mabao 8-1.

Lakini hali ya hewa ya Kitwe ni mawingu ya hapa na pale, manyunyu na joto la wastani. Uwanja ambao Simba watachezea mchezo huo wa Jumamosi jioni unaingiza mashabiki 10,000.

 

Ni uwanja mdogo ambao umepewa jina la Nkana na timu hiyo hupenda kuchezea mechi zao hapo kwa madai kwamba ndiko machinjioni kwao na mgeni huwa hachomoki.

Simba ambayo tayari ilishata-nguliza mashu-shushu wao kabla ya timu kutua jana Jumatano, imeanza kuhofiwa katika maeneo mbalimbali ya Kitwe kutokana na rekodi zake na haswa uwepo wa Cleytus Chama ambaye ni staa wa Zambia.

Loading...

Toa comment