The House of Favourite Newspapers

Simba Kutua Dar Jumatano Wakitokea Sauzi

KIKOSI cha Simba kinarejea nchini siku Jumatano ya Julai 31,  kutokea Afrika Kusini baada ya kumaliza kambi yake ya wiki mbili ya maandalizi ya msimu mpya.

Kikosi hicho kipo kwenye maandalizi chini ya kocha wake Patrick Aussems ambaye aliipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita. Katibu wa Simba, Dkt Anold Kashembe alisema kuwa kikosi hicho kitarejea hapa nchini siku ya Jumatano wiki ijayo tayari kwa Simba Day.

 

Kiongozi huyo alisema kuwa timu hiyo itarejea kwa ajili ya Simba Day ambayo itafanyika Agosti 6 na mipango yake ya kimataifa.

 

“ Kwa hiyo timu itarejea hapa nchini kwa ajili ya tukio hilo na wakimaliza ndipo wataanza safari yao ya kwenda Beira Msumbuji kujiandaa na mchezo ule wa kimataifa tunaamini kuwa maandalizi yetu ni mazuri,”alisema Katibu.

Comments are closed.