The House of Favourite Newspapers

Simba: Machi 2 tunakwenda kuandika historia nyingine

0

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally amesema, hawajawahi kushindwa mechi za kuamua hatma yao kwenda Robo Fainali.

Amewataka wanasimba kujitokeza kwa wingi Jumamosi hii Machi 2, 2024 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa kuhakikisha wanammaliza Jwaneng Galaxy kwa kuibuka na ushindi na kusonga hatua ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika.

“Mechi Kama hii ambayo tunakwenda kuicheza Jumamosi, Simba tumeshacheza mechi za aina hiyo tano (5) na zote tulipa ushindi.

“Hatujawahi kushindwa kupata ushindi katika mechi ya hatua kama hii ya kutupeleka hatua ya robo fainali, na Machi 2, 2024 tunaenda kuandikisha historia nyingine,” Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally.

Leave A Reply