The House of Favourite Newspapers

SIMBA SC YAITUNGUA JKT TANZANIA DAKIKA YA 90+7

Timu ya Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi baada ya kupata bao zikiwa zimebaki sekunde chache mpira kumalizika kupitia kwa Hassan Dilunga.

Mchezo huo ambao tangu mwanzo ulikua wa piga nikupige huku mashambulizi yakiwa ni kwa pande zote, Simba wamekosa mabao mengi huku JKT nao wakikosa mabao mengi lakini bahati ilikuwa upande wa Simba.

Bao la Simba limefungwa ndani ya dakika 7 za nyongeza (90’+7) na kuendelea kuwasogelea Yanga ambao wanaongoza Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 77 na michezo 33, huku Simba ambao wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 71na michezo 28, mbele ya Azam waliopiga jana na Yanga na kubaki nafasi ya tatu wakiwa na pointi zake 66 na michezo 33.

Picha na Musa mateja | GPL

Comments are closed.