The House of Favourite Newspapers

Simba vs Namungo…Moto Utawaka Leo Sheikh Amri Abeid, Arusha

0

JOTO la mtanange wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na Namungo, limepanda ambapo leo Jumapili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, moto utawaka wakati timu hizo zikipambana.

 

Simba na Namungo zinatarajia kufungua pazia la msimu wa 2020/21 kwa kucheza mechi hiyo ambapo baada ya hapo, Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuanza Septemba 6, mwaka huu.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba, juzi Ijumaa usiku walifi ka jijini Arusha wakitokea Dar kwa ajili ya mchezo huo, huku Namungo nayo ikifi ka siku hiyohiyo.

 

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, alisema: “Tunatarajiwa kuwakosa baadhi ya wachezaji wetu kutokana na sababu mbalimbali ambao ni wa Namungo, Hitimana Thiery, amesema:

“Tumejipanga kwa ajili ya mchezo huo, tumefi ka huku kwa kuchelewa sana, tuliingia jana (juzi) usiku, sehemu tuliyofi kia haikuwa yenye mazingira mazuri, ikabidi tuhame na kutafuta sehemu bora.“Kwa namna ninavyoona, siwezi kusema moja kwa moja kwamba tunaweza kushinda mechi hii.

 

”Hii itakuwa ni mara ya nne kwa timu hizo kukutana kwenye historia yao ambapo msimu uliopita wa 2019/20 zilikutana mara tatu. Mara mbili kwenye ligi na moja fainali ya FA. Matokeo ya mechi hizo yalikuwa hivi; Simba 3-2 Namungo, Namungo 0-0 Simba na Simba 2-1 Namungo.

Leave A Reply