The House of Favourite Newspapers

Simba wa Mwanza watua Shinyanga kupambana

Kikosi cha timu ya Simba SC.

VIGOGO wote wa Simba Kanda ya Ziwa, wametua Shinyanga kuongeza nguvu dhidi ya Stand United. Katibu mkuu wa matawi ya Simba mkoa wa Mwanza, Philbert Kabago amesema uongozi wa matawi hayo jijini hapa kwa kushiriniana na baadhi ya wanachama wa timu hiyo tayariwamewasili mkoani Shinyanga kwa lengo lakuongeza nguvu.

 

Kabago amesema; “Mara nyingi timu yetu inapokuja kanda ya ziwa huwa inakamiwa sana kwenye michezo yake lakini kwa jinsi ambayo tumejipanga tunaamini hakuna wa kutuzuia.”

 

“Simba kila inapokwenda ni kama inakuwa nyumbani kutokana na kuwa na mashabiki kila kona ya nchi hivyo tunawaomba wapenzi na mashabiki wa timu yetu wajitokeze kuishangilia timu yetu ili iweze kupata pointi tatu muhimu dhidi ya Stand United,” aliongeza Katika mchezo wa msimu wa mwaka 2017/18 tmu ya Simba ilipata ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Stand United. Msimu huu zinacheza leo Jumapili

Comments are closed.