The House of Favourite Newspapers

Simba waacha basi Dar, wapanda daladala

0

SONY DSC

Na Ibrahim Mussa
Dar es Salaam
KATIKA hali isiyo ya kawaida, juzi Jumatano wachezaji na benchi zima la ufundi la Simba waliingia kwenye Uwanja wa Majimaji, Ruvuma wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Coaster ambalo ni daladala linalofanya safari zake Stendi Kuu kwenda Peramiho mkoani humo baada ya basi lao kuliacha jijini Dar.

Simba ambayo juzi ilicheza dhidi ya Majimaji na kutoka suluhu, iliondoka Dar, Jumatatu wiki hii kwa usafiri mwingine huku kukiwa hakuna taarifa za uhakika juu ya basi lao ambalo walipewa na wadhamini wao, Kampuni ya Bia (TBL). simba-sports-club-kikosiKikosi cha Simba

Mchezaji mmoja wa kikosi cha kwanza wa Simba aliliambia gazeti hili kuwa basi hilo liliharibika, ndiyo maana hawakulitumia kusafiri.
Gazeti hili lilipowasiliana na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara juu ya suala hilo, alikuwa mkali na kusema:
“Yaani nyie waandishi wa siku hizi ni wa ajabu sana, mnaokota habari kwenye mitandao halafu mnazileta hapa, kwani nini tatizo sisi kupanda hilo basi, tatizo lake ni nini, kwa hiyo kwako unaona ni tatizo kubwa.”
Baada ya kutoa kauli hiyo Manara alikata simu.

Leave A Reply