The House of Favourite Newspapers

Simba Walivyosepa Dar leo Kuelekea Algeria, Kukipiga na JS Saoura

Kikosi cha wachezaji 20 wa Simba waliondoka leo Jumanne kuelekea Algeria kwa mechi ya marudiano dhidi ya JS Saoura itakayochezwa Machi 9.

Wachezaji 20, waliondoka ni Aishi Manula, Zana Coulibaly, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Mohammed Hussein, Pascal Wawa, Poul Bukaba, James Kotei, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, Cletus Chama, Rashid Juma, Abdul Selemani, Bocco, Maddie Kagere, Adam Salamba.
Wengine Deo Munishi, Asante Kwasi, Mohammed Ibrahim na kiungo fundi Haruna Niyonzima.


Akizungumzia kuondoka kwa Simba bila ya Okwi, nahodha Bocco alisema hata kama kuna baadhi ya mchezaji anakosekana bado malengo yao ya kufanya vizuri yapo pale pale.

Alisema hilo la kukosekana kwa baadhi ya wachezaji halipo chini yangu kwani ninaimani kila mchezaji ambaye atapata nafasi ya kucheza atatimiza majukumu yake.


“Kwetu wachezaji tumepata muda wa kujiandaa vizuri na kwenda kushindana katika mechi na JS Saoura malengo yetu yakiwa ni palepale kufanya vizuri,” alisema Bocco.


“Tunafahamu tunakwenda kucheza na timu ambayo itakuwa imebadilika na si ile ambayo tulicheza nayo katika mechi ya kwanza hapa nyumbani.

“Wachezaji wote waliokuwepo wanamorali ya hali ya just kubwa tunaomba Watanzania watuombee ili twende kulifanya na kulitimiza lile ambalo lipo katika mioyo yetu,” alisema Bocco.

 

Comments are closed.