The House of Favourite Newspapers

SIMBA WASHINDI WA TATU UHAI CUP (UNDER 20)

Timu ya vijana cha Simba kimefanikiwa kuwa mshindi namba 3 wa michuano ya Vijana wa Timu za Ligi Kuu Bara chini ya Umri wa MIaka 20 (Uhai CUP – Under 20) ilivyokuwa ikifanyika Uwanja wa Chuo kikuu jijini Dodoma baada ya ushindi  wa mabao 4-3 kwa njia ya matuta dhidi ya Azam FC.

Ushindi huo umepatika mara baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1 na kuamuriwa changamoto ya mikwaju ya penati kuchukua hatua yake.

Bao la Simba ndani ya dakika 90 lilifungwa na Yahya Mbegu katika dakika ya 7 ya mchezo na la kusawazisha kwa Azam likiwekwa kimiani na Paul Peter kwenye dakika ya 33.

Baada ya dakika 90 kumalizika na upigaji wa penati kuanza, Simba walifanikiwa kupata 4 huku Azam wakipata 3.

Comments are closed.