The House of Favourite Newspapers

Simba Waua Wanafunzi Watatu Arusha

0

WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Ngoile wilayani Ngorongoro, Mkoa wa Arusha, wameuawa kwa kushambuliwa na Simba, walipokuwa wanatafuta mifugo yao iliyopotea porini.

 

Taarifa ya tukio hilo imetolewa jana Alhamisi, tarehe 5 Agosti 2021 na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, akizungumza na wanahabari.

 

Kamanda Masejo amesema, wanafunzi hao ambao ni Olobiko Metui (10), Ndaskoi Sangu (9) na Sanka Saning’o (10), waliuawa tarehe 3 Agosti mwaka huu.

 

Amesema wanafunzi hao waliokuwa darasa la tatu, walienda porini kuitafuta mifugo hiyo, wakitokea nyumbani kwao baada ya kurudi kutoka shule.

 

Kamanda Masejo amesema, mwanafunzi mmoja, Kiambwa Lektony (11), alifanikiwa kutoroka katika mashambulizi ya Simba, ambaye anapatiwa matibabu katika Zahanati ya Kata ya Olbalbal, mkoani humo.

 

“Miili ya marehemu wote imefanyiwa uchunguzi wa kidaktari na imeshakabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi,” amesema Kamanda Masejo.

 

Kamanda Masejo amewataka wafugaji wasiwape watoto majukumu ya kuchunga mifugo, hasa katika maeneo ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za wanayamapori, ili kuokoa maisha yao.

 

Leave A Reply