The House of Favourite Newspapers

Simba Yaichapa Mbeya City, Yasogea Mpaka Nafasi ya Pili

0

TIMU ya Simba imefanikiwa kuzoa pointi tatu muhimu ugenini, dhidi ya Mbeya City baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu bara uliochezwa leo Desemba 13 kwenye dimba la Sokoine, Jijini Mbeya.

 

Bao pekee kwenye mchezo huo limefungwa na nahodha John Bocco dakika ya 32, akipokea pasi murua ya Clatous Chama, kabla ya kuwazunguka mabeki wa Mbeya city na kukwamisha mpira kimiani.

 

Katika mchezo huo nyota Luís Jose Miquissone hakucheza lakini mshambuliaji ambaye alikuwa majeruhi, Chris Mugalu aliingia katika kipindi cha pili kuchukua afasi ya Bocco.

 

Baada ya matokeo ya mchezo huo myama simba amesogea mpaka nafasi ya pili akifikisha alama 29 baada ya kucheza michezo 13,  Mbeya City anasalia na alama 12 baada ya kucheza michezo 14.

 

Timu ya Wananchi Yanga wanaongoza ligi kwa pointi 35 baada ya kushuka dimbani mara 15, na Azam Fc nafasi ya tatu na alama 27.

Leave A Reply