The House of Favourite Newspapers

Simba Yaishushia Moto Mbeya City, Yaipiga 4G

KIKOSI cha Simba leo kimelipa kisasi cha kupoteza mchezo wake mbele ya Mwadui FC kwa kufungwa bao 1-0 uwanja wa Kambarage kwa kuichapa mabao 4-0 Mbeya City. uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru.

 

Mchezo wa leo ulikuwa ni wa ushindani mkali ambapo iliwalazimu Simba kusubiri mpaka dakika ya 8 kuandika bao la kwanza kupitia kwa Meddie Kagere ambaye alifunga bao hilo kwa penalti baada ya Miaji Athuman kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la 18.

Kazi haikuishia hapo zikiwa zimebaki dakika tatu kwenda muda wa mapumziko dakika ya 43 kiungo Clatous Chama alifunga bao la pili akiwa nje ya 18 akimalizia pasi ya Ibrahim Ajibu mpira uliomshinda mlinda mlango wa Mbeya City na kuifanya Simba kwenda vyumba vya mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0.

 

Kipindi cha pili Simba ilianza kwa kufanya mabadiliko kwa kumtoa Miraj ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Francis Kahata mambo yakazidi kuwa magumu kwa Simba ambapo Mbeya City ilichangamka kutafuta mabao ya kusawazisha huku ikimtumia mshambuliaji wao Peter Mapunda.

Iliawalizimu Simba kusubiri mpaka dakika ya 78 kufunga bao la tatu kupitia kwa Sharaf Shiboub aliyemalizia pasi ya Ajibu kabla ya dakika ya 83 Ajibu kumpisha Deo Kanda ambaye alichukua dakika nne kuandika bao la nne akimalizia pasi ya Clatous Chama.

 

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 21 baada ya kucheza mechi nane imeshinda saba na imepoteza mechi moja huku Mbeya City ikiwa imeshinda mechi moja kati ya tisa iliyocheza mpaka sasa na imetoa sare tano na kupoteza mechi tatu.

Comments are closed.