The House of Favourite Newspapers

Simba Yakomalia Dili La Kiungo Mtogo Kumalizana na Moses Phiri

0
Novon Efoe

HUENDA muda wowote kuanzia leo, Simba inaweza kumalizana na straika wao raia wa Zambia, Moses Phiri ili kumpisha kiungo mkata umeme raia wa Togo, Novon Efoe.

Msimu uliopita, Efoe alikuwa akikipiga kwenye Klabu ya ASKO Kara ya kwao Togo, ambayo alijiungana nayo Novemba 1, 2020, akitokea AS Togo Port.

Chanzo chetu kutoka Simba, kimeliambia Spoti Xtra kuwa, uongozi wa Simba leo Jumapili unatarajia kukaa mezani na Phiri wamalizane ili wapate nafasi ya kumuingiza kiungo huyo.

“Jumapili kuna uwezekano mkubwa wa kumaliza mazungumzo na Phiri ili aweze kwenda kwa mkopo Zanaco United na nafasi yake tuitumie kuleta kiungo mpya, ambaye atasaidiana na Sadio Kanoute pamoja na Fabrice Ngoma.

“Tunaendelea kumshawishi Phiri akubali kuondoka maana hakutaka tangu mwanzo na kwamba anataka tumuache aende bure jambo ambalo hatujaafikiana, hivyo kama tutakubaliana kumtoa kwa mkopo basi kuanzia Jumatatu ijayo tutamtangaza kiungo mpya mkata umeme,” kilisema chanzo hicho.

Inaelezwa kwamba, Simba imekuwa ikitafuta kiungo mwingine mkabaji licha ya kumsajili Fabrice Ngoma, hiyo ni katika kuimarisha kikosi chao baada ya kuondoka kwa Jonas Mkude.

Katika nafasi hiyo ya kiungo mkabaji, ndani ya Simba hivi sasa inachezwa na Mzamiru Yassin, Sadio Kanoute na Fabrice Ngoma ambaye ni usajili mpya.

STORI NA MUSA MATEJA

ALI KAMWE AWAPONDA SIMBA KUONGOZA LIGI – ”UTARATIBU WANAUJUA, HATA WACHEZE MECHI 5 MFULULIZO”…

Leave A Reply