The House of Favourite Newspapers

Simba yampa Kiongera nyumba 3 Dar

0

kiongera Paul Kiongera.

Nicodemus Jonas, Dar es Salaam
SUPASTAA! Katika kile kilichoonekana Mkenya, Paul Kiongera analelewa kama mfalme wa Simba, uongozi wa klabu hiyo umempa nyumba tatu achague mwenyewe aishi wapi.

Nyota huyo ambaye alirejea kikosini wiki mbili zilizopita akitokea KCB ya Kenya alipokuwa kwa mkopo, hata hivyo mpaka wikiendi hii alikuwa hajajua pa kuishi kutokana na kuwa kambini tangu amejiunga nao huko Zanzibar kabla ya kuweka kambi huko maeneo ya Changanyikeni, Dar kujiandaa dhidi ya Azam, mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 Jumamosi iliyopita.

Mratibu wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, suala la Kiongera ataishi wapi hawana presha nalo kwani tayari kuna nyumba tatu zilizo wazi, hivyo ni yeye kuchagua aishi wapo na nani.

“Kuna nyumba tatu pale Shekilango zipo wazi mpaka sasa, atachagua mwenyewe aishi wapi na akina nani. Mfano kuna sehemu alikuwa anaishi Simon Ssserunkuma, bado haina mtu akipenda atahamia hapo,” alisema Gazza.

Awali, straika huyo kipenzi cha Wanasimba, alikuwa akiishi Chang’ombe lakini kwa sasa nyumba hiyo ina watu wengine, akiwemo daktari wao, Yassin Gembe.

Leave A Reply